Kutoa mimba ni haramu Zimbabwe lakini mwanamke anaweza kuruhusiwa kufanya hivyo ikiwa mimba yake imetokana na kitendo cha ubakaji au ikiwa inahatarisha maisha ya...
mwanamke huyo.
Mtoto wa mwanamke huyo sasa ana umri wa miaka minane na anaenda shule.
Mwandishi wa BBC mjini Harare Brian Hungwe anasema kuwa mahakama ilisema kuwa mafadhaiko aliyoyapata mwanamke huyo kutokana na mimba yalitarajiwa na kwa hivyo madaktari walipaswa kumshauri mwanamke kutumia tembe za kuzuia mimba siku tatu baada ya mwanamke huyo kubakwa mwaka 2006.
Badala yake madaktari walimshauri mwanamke kuenda kwa polisi na hivyo kuifanya mimba kukomaa.
Kadhalika mahakama imeitaka mahakama nyingine kuamua kiwango cha fidia atakacholipwa mwanamke huyo.
Mwenyewe ametaka kulipwa dola 42,000 za kimarekani kugharamia malezi ya mtoto huyo, ingawa mahakama ilitupilia mbali ombi lake.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.