Friday, March 14, 2014
0

Mahakama nchini Ujerumani imemhukumu rais wa klabu bingwa Ulaya, Bayern Munich, Uli Hoeness, kifungo cha miaka mitatu na miezi sita jela kwa kukwepa kulipa kodi.
Nyota huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 62 alikiri kuitapeli mamlaka ya...
kutoza ushuru ya Ujerumani mamilioni ya Euro huku akiweka akiba ya fedha zake kisiri kwenye akaunti ya benki ya Uswizi.
Licha ya wakili wake kuiomba mahakama kutomwadhibu Bw Hoeness kwa sababu ya kujisalimisha kwake, mahakimu waliafikia kwamba Hoeness hakukiri kikamilifu.
Hapo awali Hoeness alishtakiwa kwa kukwepa kulipa ushuru wa euro milioni 3.5 (£2.9m; $4.9m) lakini baadaye akakiri kuwa hajawahi kulipa milioni nyingine 15.
Hatimaye Alhamisi, korti ilibaini kuwa alikosa kulipa ushuru wa jumla ya euro milioni 27.2.
Hoeness amesema hatakata rufaa dhidi ya uamuzi huo
Hata hivyo Hoeness atabakia kuwa huru hadi uamuzi wa mwisho kabisa utakapotolewa.

0 comments:

Post a Comment

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA

66205