Utafiti mpya kutoka ulaya na marekani kazkazini
unasema kuwa,kupigwa marufuku kwa uvutaji wa sigara hadharani
kumesababisha kushuka kwa viwango vya wanawake kujifungua mapema kabla
ya muda wao kwa asilimia 10.
Idadi ya watoto waliolazwa hospitalini kutokana
na ugonjwa wa pumu pia imepungua kwa asilimia 10% katika maeneo ambayo
uvutaji sigara hadharani umepigwa marufuku kulingana na wanasayansi
kutoka chuo cha Edinburgh nchini Scotland.
Mmoja ya waanzilishi wa utafiti huo Prof Aziz
Sheikh ambaye ripoti ya...
utafiti wake imechapishwa katika jarida la
matibabu duniani Lancet,anasema kuwa mataifa yasio na marufuku hiyo
yanapaswa kutilia maanani matokeo hayo kwaajili ya kizazi chao cha
baadaye.
Kwa sasa ,sheria dhidi ya uvutaji sigara zinaathiri asilimia 16 ya idadi ya watu dunaini.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.