swali lililoulizwa na Waziri mkuu wa mpito wa Ukraine, Arseniy Yatsenyuk.
Kwingineko, mashariki mwa Ukraine mjini Donetsk, mtu mmoja ameuawa wakati wa vurugu za waandamanaji mahasimu, maofisa wameeleza.
Watu kadhaa pia wamejeruhiwa wakati mamia ya waandamanaji wanaoiunga mkono Urusi walipopambana na waandamanaji wanaoiunga mkono Kiev.
Machafuko haya yanaelezwa kuleta athari kubwa tangu kuanguka kwa Rais wa Ukraine Viktor Yanukovych, tarehe 22 mwezi Februari.
Kumekuwa na hali ya mvutano mkubwa wa kidiplomasia wakati kura ya maoni ikitarajiwa kupigwa na Raia wa Crimea.
SOURCE BBC SWAHILI
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.