Rwanda iliwafurusha wanadiplomasia sita wa Afrika Kusini baada ya serikali ya Afrika Kusini kuwafukuza wafanyakazi watatu wa ubalozi wa Rwanda na mmoja wa Burundi nchini humo baada ya kuwahusisha na njama ya kutaka kumuua Nyamwasa.
Wakati huohuo, Mjumbe maalum wa Rais Barack Obama katika kanda ya maziwa makuu, Russ Feingold amesema kuwa nchi za Rwanda na Afrika Kusini hazina budi kumaliza mzozo kati yao kwa njia za kidiplomasia.
Mjumbe huyo aliyasema hayo mjini Kigali baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Feingold amesema Marekani inafuatilia kwa karibu karibu kundi la FDLR akilitaja kama moja ya makundi hatari katika eneo hilo la maziwa makuu.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.