kuhalalisha uuzaji wa bangi kwa matumizi wa starehe.
Utawala wa jimbo hilo umesema kuwa ushuru huo utatumiwa kujenga shule.
Ruhusa uuzaji wa bangi na ushuru utaongezeka maradufu, ni moja kati ya masuala yaliyopogiwa debe na wanaharakati wanaunga mkono matumizi ya bangi katika jimbo Colorado.
Bangi yenye dhamani ya dola milioni kumi na nne iliuzwa Januari pekee, wakati sheria hiyo ilioidhinishwa.
Wapiga kura waliidhinisha sheria hiyo baada ya kura ya maoni katika majimbo ya Colorado na Washington licha ya kuwa serikali ya Marekani, ingali imeorodhesha bangi kama dawa ya kulevya.
Jimbo la Colorado, ilikuwa jimbo la kwanza kuruhusu maduka kuuza bangi na inatoza ushuru wa uugizaji na uuzaji.
Hata hivyo bado kuna mjadala mkali si tu kuhusu swala hilo nyeti la kuruhusu uzwaji bangi, lakini pia khusu ni mradi upi utafadhiliwa baada ya mradi huo wa ujenzi wa shule kukamilika .
Baadhi ya raia nao wanataka fedha hizo kutumiwa kuthibiti uuzaji na ukuzaji wa bangi nao wengine wakipendekeza kutumiwa kwa kampeini ya kuwahimiza watoto kutojiingiza katika tabia ya uvutaji bangi na pia kupigia debe kampeni ya kuwashawishi watu wasiendeshe gari wakiwa wamevuta bangi.
![]() |
Bangi ikichambuliwa ili kuweza kuanza kupimwa.. |
![]() |
Hata kulimwa sasa inalimwa na kutunzwa kitaalamu zaidi.. mmmhh!! SOURCE BBC SWAHILI |
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.