Mahakama kuu ya ICC, kupitia mwendesha mashitaka Fatou Bensouda, imekuwa ikiitaka serikali ya Kenya kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuendesha kesi zinazowakabili Rais Kenyatta na naibu wake bwana Ruto.
Hii ni mojawapo ya sababu kuu ya kubadili tarehe ya kusikizwa kwa kesi hii.
Upande wa mashitaka umesema kuwa unaipa Kenya muda wa...
ziada ili kutafuta na kuwasilisha baadhi ya stakabadhi za benki zinazohitajika katika kesi hiyo.
Kumekuwa na malalamishi kutoka kwa upande wa mashitaka kuwa serikali ya Kenya inalenga kuzuia stakabadhi hizo kufikishwa mahakamani jambo ambalo mawakili wa bwana Kenyatta wamekanusha.
Miongoni mwa yale yanayohitajika kotini ni pamoja na taarifa ya maelezo ya fedha anazomiliki bwana Kenyatta.
Kesi hii imekumbwa na matatizo ya mashahidi kujiondoa na shutuma za mahakama hii kuonea viongozi wa bara Afrika.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.