Nahodha mkuu haijabainika alikuwa wapi wakati wa tukio ila inadhaniwa feri hiyo iligonga mwamba na kupinduka kwa haraka baada ya shehena yake kuegemea upande mmoja.
Wachungizi sasa wanaelekeza juhudi zao kubaini kwanini Nahodha wa Sewol hakuwa kwenye usukani na pia kwanini baada ya tukio la kwanza abiria walikanywa wasiruke baharini ilikuokoa nafsi zao kama ilivyodesturi chombo kikigonga mwamba ?
Kiongozi wa Mashtaka ya umma nchini Korea bwana Park Jae-Eok amesema kuwa....
nahodha mkuu Lee Joon-seok,atakuwa na swali la kujibu .
Watu 26 pekee ndio wamedhibitishwa kufariki kufikia sasa, huku 179 wakiokolewa.
Makundi ya waokoaji wamefanikiwa kuingia ndani ya feri hiyo kwa mara ya kwanza leo asubuhi baaha ya kutoboa shimo upande wa juu wa chombo hicho kilichozama.
Waokoaji walikuwa wameshindwa kuingia ndani ya feri hiyo baada ya bahari kuchafuka.
Mamia ya jamaa na marafiki ya wahasiriwa wamelalamikia ukosefu wa habari za uokaji .
Wengi wamekuwa wakivumilia hali mbaya ya hewa wakiomba kuruhusiwa kusubiri wapendwa wao ufukweni.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.