Mamake mwathiriwa alimzaba kofi mtuhumiwa na kisha kumasamehe dakika chache kabla ya kunyongwa
Mtu mmoja aliyehukumiwa kifo kwa
kunyongwa nchini Iran baada ya kupatikana na hatia ya mauaji, ameponea
chupuchupu baada ya kusamehewa na mamake mwathiriwa.
Mama huyo alimsamehe mtuhumiwa dakika chache tu kabla ya kuwekwa kamba shingoni.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Iran.
Picha za tukio hilo zilipigwa moja kwa moja na
mpiga picha mmoja aliyenasa kila hatua ya tukio hilo ambalo
liliwashangaza wengi nchini Iran na......
duniani kote.
Balal alimuua kwa kumdunga kisu Abdollah Hosseinzadeh miaka saba iliyopita
Shirika la habari la ISNA nchini Iran liliripoti
kuwa mtuhumiwa huyo, kwa jina Bilal, alihukumiwa kifo baada ya kumuua
kijana mmoja Abdollah Hosseinzadeh, wakati wawili hao walipokuwa
wanapigana katika soko moja mjini Nour miaka saba iliyopita.
Bilal alifikishwa katika sehemu ya kunyongewa akiwa amefunikwa macho yake tayari kwa hukumu kutekelezwa siku ya Jumanne.
Lakini dakika ya mwisho kabla ya kunyongwa,
mamake mwathiriwa Samereh Alinejad, alimwambia kuwa amemsamehe baada ya
kuhutubia umati uliofika kushuhudia hukumu hiyo , kisha akamzaba kofi
Bilal kabla ya Bilal kunusurika kifo.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.