Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 18 alikuwa na mimba ya miezi mitatu wakati alipovamiwa na genge la wanaume na kubakwa.
Wanaume watatu waliokiri kufanya mapenzi na mwanamke huyo na wawili waliosambaza kanda hiyo wataadhibiwa kwa kuchapwa mijeledi.
Kwa mujibu wa shirika moja la kutetea haki za wanawake (Strategic Initiative for Women) katika upembe wa Afrika (SIHA),watatu hao watapokea viboko miamoja kila mmoja kama adhabu ya kosa la zina wakati wawili wakiadhibiwa mijeledi 40 kwa kusambaza kanda yenye picha chafu.
Mwanamke huyo alifungwa jela mwezi mmoja lakini adhabu hiyo ilifutiliwa mbali kwa sababu ya ujauzito wake. Pia alitozwa faini ya dola 880.
Kadhalika alikabiliwa na makosa ya zina pamoja na ukahaba, ambayo adhabu yake ni kifo kwa kupigwa mawe nchini Sudan. Lakini hakupata adhabu hiyo kwani alishawishi mahakama kuwa ametalakiana na mumewe.
Inaarifiwa mwanamke huyo alikuwa anatafuta nyumba ya kupangisha wakati alipohadaiwa na kuingizwa ndani ya nyumba moja ambapo wanaume hao walimbaka mjini Omdurman.
Mwanamke huyo huenda akarejeshwa nchini Ethiopia.
Shirika hilo limelaani adahabu dhidi ya mwanamke huyo likisema kuwa litawazuia wanawake kuripoti visa vya ubakaji.
SOURCE BBC SWAHILI
Kwa style hiyo inabidi waache kulalamika maana Ni uonevu
ReplyDeleteKhatariii Dada Esther..
ReplyDeleteKhatariii Dada Esther..
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.