Bustani hiyo iliyopo mjini Southend nchini Uingereza, imeweka ilani zinazowaomba wanaume wasivue mashati yao, na kwamba watakao patikana watafukuzwa.
Mkurugenzi mkuu, Marc Miller, amesema anataka wanaume waonyeshe "ustaarabu".
'Kuilenga Familia'
Zaidi ya watu 100 walivua nguo ili kuipanda bembea hiyo ijulikanayo kama......
Green Scream mnamo 2010.
Miller anasema: "Katika miaka ya hivi karibuni, tumekuwa tukiongeza idadi ya vijana na wanaume ambao huvua mashati yao ili kupata joto la jua kwa wingi. Hilo ni sawa kabisa lakini katika mazingira yanayofaa".
"Tunajaribu sana kufanya biashara inayoivutia familia na sio kila mtu anavutiwa kuona vifua wazi".
Pamoja na kuwa na idadi kubwa duniani ya watu wasio vaa nguo, Adventure Island pia ilijaribu kuweka rekodi mpya ya kuwa na watu wengi wanaocheza mpira wa gofu wakiwa uchi, mnamo mwaka 2012.
Msemaji mmoja anasema michezo yote hufanyika faraghani.
"Wanaohudhuria michezo hiyo ni waliojisajili kushiriki, ili kuchanga fedha nyingi za misaada ya kukabiliana na magonjwa kama saratani ya matiti na ya uume," alisema.
"Marufuku hiyo imetolewa wakati bustani imefunguliwa kwa umma."
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.