Shirika la habari la Uingereza, Reuters, limewakariri watu walioshuhudia tukio hilo wakisema mabasi mawili yaliyokuwa yamejaa abiria yalilipuliwa.
Mmoja wa mashuhuda wa shambulio hilo, Badamsi Nyanya ameiambia BBC kuwa ameona miili 40 ikiondolewa.
"Asubuhi hii kulikuwa na mlipuko katika eneo la.....
maegesho ya magari ya Nyanya Motor Park," anasema Manzo Ezekiel wa Wakala wa Usimamizi wa Taifa wa Majanga.
Vikosi vya uokoaji tayari vipo katika eneo la tukio.
Shuhuda mwingine Bi Mimi Daniels, ambaye anafanya kazi mjini Abuja, anasema: "nilikuwa nasubiri basi niliposikia mlipuko mkubwa halafu nikaona moshi," ameiambia Reuters.
"Watu walikuwa wakikimbia ovyo kutokana na taharuki."
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.