Mtu mmoja ameripotiwa kuuawa na
wengine wengi kujeruhiwa katika mapigano katika mji wa Mombasa pwani ya
Kenya. Polisi walipambana na vijana walioingia katika Msikiti wa Swafaa
eneo la Kisauni na mpaka sasa zaidi ya vijana 400 wanashikiliwa tangu
kuanza kwa msako huo, mapema wiki hii.
Mwandishi wa BBC, Emmanuel
Igunza anasema Msikiti huo ulifungwa jana baada ya polisi kuuvamia
Jumatano, ambamo walipata magruneti, mabomu ya petroli na silaha
nyingine. Hali ya wasi wasi bado imetanda katika mji huo wa pwani.
Serikali imekwishafunga misikiti minne ambayo wanasema ina uhusiano wa
watu wenye misimamo mikali ya imani ya kidini.
Pamoja na kukamata silaha mbalimbali, polisi pia
walikamata bendera nyeusi, alama ya kuunga mkono kundi la kigaidi la
Al-Shabab la nchini Somalia
Awali polisi mjini Mombasa
pwani ya Kenya walisema wamepata silaha nyingine zaidi yakiwemo mabomu
katika msikiti wa tatu ambao ulifanyiwa upekuzi Msako huo katika
msikiti wa Swafaa mtaani Kisauni unakuja baada ya msako mwingine wa
Jumatatu ambapo polisi pia walipata silaha ndani ya msikiti ambao
wanasema hutumika kutoa mafunzo yenye itikadi kali. Mtaa wa Kisauni ndiko vijana waliokuwa wamejihami kuwadunga visu watu wanne na kuwaua. Pia waliwashambulia kwa silaha nyingine. Waziri
wa usalama wa ndani, Joseph Ole Lenku anasema kuwa msako huo ulifanywa
katika misikiti ambayo hutumiwa na watu wanaoeneza itikadi kali za
kiisilamu kwa vijana ambao inadaiwa wanajiunga na kundi la wapiganaji wa
kiisilamu la Al Shabaab nchini Somalia. Viongozi wa kiisilamu
wamelaani misako hiyo katika Misikiti wakisema kuwa itachochea zaidi
vijana kuendeleza itikadi kali za kidini
Mwanamke mmoja nchini Sweden amejifungua mtoto kutokana na kizazi alichowekewa kupitia upasuaji.
Mwanamke
huyo mwenye umri wa miaka 36 alizaliwa b...Read more
Basi la kwanza nchini Uingereza linalotumia kinyesi na uchafu unaotokana na chakula limeanza safari yake ya kwanza.
Bio
Bus,lenye viti 40 na amba...Read more
Timu ya soka ya Ivory Coast huenda
ikakabiliwa na vikwazo baada ya mashabiki wake kuvamia uwanja mjini
Abidjan baada ya kupata fursa ya kuwakil...Read more
Ripoti kutoka Magharibi mwa Afrika zinasema kuwa sherehe za Eid Ul Adhaa zimeathiriwa vibaya na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Nchini Guinea maeneo ...Read more
Polisi nchii Tanzania wanasema watu 7 wameuawa kwa kuchomwa katika eneo la Kigoma magharibi mwa nchi hiyo kwa tuhuma za uchawi.
Nyumba za marehemu...Read more
Wafungwa wawili wamepigwa risasi walipokuwa wakijaribu kutoroka kutoka katika mahakama moja nchini Afrika Kusini.
Afisa
mmoja kutoka wizara ya sh...Read more
0
comments:
Post a Comment
Click to see the code! To insert emoticon you must added at least one space before the code.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.