UTANGULIZI:
Yeremia
25:34-37 “Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na
kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za.....
kuuawa
kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama
chombo cha anasa. Nao wachungaji
watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi
hawataokoka. Sauti ya kilio cha wachungaji,
na sauti ya kupiga yowe kwao walio hodari katika katika kundi, kwa maana BWANA
anayaharibu malisho yao. Na mazizi yenye
amani yamenyamazishwa, kwa sababu ya hasira kali ya BWANA”.
Katika mkesha
wa maombi ya KANISA LA PENTEKOSTE
TANZANIA (KLPT) Parish ya Mbezi Luis,
Jimbo la Kinondoni Dar Es Salaam, uliofanyika usiku wa tarehe 12 kuamkia tarehe
13 mwezi Oktoba, 2012 hapa Parishini, Neno la BWANA lilishuka na kunilenga mimi
MCHUNGAJI BENT M. DONGWE likisema:
“Nakutuma
wewe Mchungaji BENT M. DONGWE,
nenda kaseme na Wachungaji na Wahubiri wa Kanisa la Tanzania kupitia vyombo vya
habari, Television, Redio na Magazeti uwaambie Bwana wa Majeshi asema hivi;
Acheni mara moja kuhubiri watu fedha Makanisani, wahubirieni watu Neno langu,
acheni kuwakata Kondoo wangu mikia, acheni kuwakusanya Kondoo wangu ili
kushibishana matumbo yenu Asema Bwana wa Majeshi”.
Ezekieli 34:1-10 “Neno
la BWANA likanijia, kusema, Mwanadamu, toa unabii juu ya wachungaji wa Israeli,
toa unabii, uwaambie, naam, hao wachungaji, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao
wachungaji wa Israeli, wanaojilisha wenyewe; je! Haiwapasiwachungaji kuwalisha
kondoo? Mnawala walionona, mnajivika manyoya, mnawachinja walionona; lakini
hamwalishi kondoo. Wagonjwa hamkuwatia
nguvu, wala hamkuwaponya wenye maradhi, wala hamkuwafunga waliovunjika, wala hamkuwarudisha
waliofukuzwa, wala hamkuwatafuta waliopotea; bali kwa nguvu na kwa ukali
mmewatawala. Nao wakatawanyika, kwa
sababu hapakuwa na mchungaji; wakawa chakula cha wanyama-mwitu,
wakatawanyika. Kondoo zangu
walitanga-tanga katika milima yote, na juu ya kila kilima kirefu; naam, kondoo
zangu walitawanyika juu ya uso wote wa dunia; wala hapakuwa na mtu
aliyewauliza, wala kuwatafuta. Basi,
enyi wachungaji, lisikieni neon la BWANA;
Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, kwa sababu kondoo zangu walikuwa
mateka, kondoo zangu wakawa chakula cha wanyama-mwitu wote, kwa sababu hapakuwa
na mchungaji, wala wachungaji wangu hawakutafuta kondoo zangu, bali wachungaji
walijilisha wenyewe wala hawakuwalisha kondoo zangu; kwa sababu hiyo, enyi
wachungaji, lisikieni neno la BWANA;
Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu ya wachungaji; nami nitawataka
kondoo zangu mikononi mwao, nami nitawaachisha hiyo kazi ya kuwalisha kondoo;
nao wachungaji hawatajilisha wenyewe tena; nami nitawaokoa kondoo zangu
vinywani mwao, wasiwe tena chakula chao”.
Warumi 16:17-18; Wafilipi 3:18-19;
Yeremia 23:10-36
Baada ya hapo
ujumbe mwingine ulishuka na kulilenga Kanisa la KLPT Mbezi Luis ukisema:
“Nimewachagua
ninyi Kanisa la Mbezi Louis, ninawatuma kutangaza MSAMAHA, waambieni watu Bwana
ameisamehe Tanzania, na haya mambo ya uchomaji wa makanisa hayatakuwepo tena,
lakini msipogeuka nitawaangamiza kwa upanga Asema Bwana wa Majeshi”.
Amosi 3:6
“Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu
wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA?”.
Isaya 1:19-20
Alisema tusipogeuka
hatakuja tena kwa njia ya kuchoma makanisa, bali kwa njia anayoijua yeye.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.