KANISA la Moravian Duniani
lenye Makao Mkuu yake nchini Norway, limeingilia kati mgogoro wa kanisa lake
Jimbo la Mashariki na Pwani Tanzania kwa kutaka kuondoa......
kesi inayowafanya
walumbane mahakamani.
Mgogoro huo ulizuka baada ya
kuondolewa nyadhifa na kusimamishwa kazi, Mwenyekiti wa Halmashauri Jimbo hilo,
Clementi Fumbo na wenzake saba.
Fumbo na wenzake saba
walifungua kesi ya madai namba 222 ya mwaka 2012, katika Mahakama Kuu ya
Tanzania Kanda ya Dar es Salaam wakipinga kuondolewa madaraka na kusimamishwa
kazi.
Katika kesi hiyo, iliyopangwa
kusikilizwa na Jaji Augustine Mwarija, Desemba 6, mwaka huu, Fumbo na wenzake
saba wanaiomba Mahakama iamuru walipwe Sh500 milioni kama fidia na gharama za
kesi.
Kanisa la Moravian duniani
ambalo makao makuu yake yapo nchini Norway limeshtushwa na mgogoro huo ambao
ulipelekwa mahakamani.
Kanisa hilo limetuma ujumbe
unaoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa kanisa hilo la Moravian dunia, Mchungaji
Nosigwe Buya na Mtendaji wake Mkuu wa Kanisa hilo, Mchungaji Jogan Boytrel.
Ilidaiwa kuwa wajumbe hao,
walipofika hapa nchini walifanya vikao tofauti tofauti na kufikia uamuzi kuwa
ifikapo Januari 15, 2013 pande zote mbili zenye mgogoro ziwe zimekwishaelewana
na kuwapelekea ripoti.
Iliendelea kudaiwa kuwa iwapo
watashindwa kufika muafaka na kuelewana Februari Mosi,2013, ujumbe huo utarudi
kutoa uamuzi na kwamba wakielewana watapewa jimbo kamili.
Katika kesi hiyo, Mchungaji
Fumbo kupitia wakili wao, Benjamini Mwakagamba wa Ofisi ya Mawakili ya BM,
wanaiomba mahakama hiyo, itamke kuwa uamuzi ambao uliowaondolea madaraka na
kuwasimamisha kazi ya kikao cha Sinodi cha Oktoba 5, mwaka 2012, kilichokaa
mkoani Morogoro ni batili kwa kuwa uamuzi huo ulitolewa bila ya wadaiwa kupewa
haki ya msingi ya kusikilizwa.
Fumbo na wenzake Mchungaji
Fred Lwitiko, Mchungaji Mosted Kibona, Mchungaji Nyambilila Lwaga, Nelson
Ngajiro, Devis Mwaikambo, Mathew Mwasiposya na Aliko Mwakatumbula kwa pamoja
wanadai kuwa wadaiwa ambao ni Mchungaji Saul Kajula, Mchungaji Clement
Mwaitebele, Halmashauri Kuu ya Jimbo la Moravian Mashariki na Bodi ya wadhamini
ya kanisa la Moravian Jimbo la Rungwe kwa pamoja na kwa nyakati tofauti walitoa
uamuzi wa kumsimamisha na kumfukuza kazi ya uenyekiti wa halmashauri ya Jimbo
la Mashariki Mchungaji Fumbo na kumuondoa kwenye nafasi ya mweka hazina
Mchungaji Lwaga.
|
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.