SIKU chache baada ya viongozi
wa dini wa madhehebu ya Kikristo nchini Malawi na Tanzania kuwasiliana kwa
lengo la kutaka wajadili mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa baina ya....
nchi hizo
mbili, Serikali ya Tanzania imezuia mjadala huo, Mwananchi imeelezwa.
Viongozi hao wa dini, Baraza
la Wakristo Tanzania (TCC) na Baraza la Wakristo Malawi (MCC) walitangaza
kujiingiza kwenye mgogoro huo wakitaka washirikishwe kama wasuluhishaji
katika kile walichoeleza kuwa mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu bila suluhu
yoyote.
Hata hivyo Serikali ya Tanzania imepinga wazo la viongozi hao kwa maelezo kuwa
suala la mzozo huo limefikishwa kwa mpatanishi maalumu ambaye amekubaliwa na
pande zote mbili.
Hivi karibuni mawaziri wa
mambo ya nje kutoka nchi zote mbili walikuwa mjini Maputo, Msumbiji kwa ajili
ya kukutana na mpatanishi wa mzozo huo, Rais wa zamani Joachim Chissano ambaye
anatazamia kuanza kazi hiyo Januari mwakani.
Kiongozi huyo wa zamani ndiye
atayeongoza jopo la viongozi wastaafu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (Sadc) kusaka suluhu ya mzozo huo ambao sasa umedumu kwa
zaidi ya miongo 6.
Hata hivyo viongozi wastaafu
wa Tanzania rais All Hassani Mwinyi, Benjamin Mkapa na yule wa Malawi Bakili
Muluzi hawataruhusiwa kushiriki kwenye jopo hilo la marais wastaafu wa nchi za
SADC.
Waziri wa mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amekaririwa akisema hoja iliyotolewa na
viongozi wa dini waliotaka kuwa sehemu ya usuluhishi kwenye mzozo huo, haina
nguvu kwani suala hilo limefikishwa kwenye ngazi ya juu zaidi.
Hivi karibuni Serikali ya
Tanzania na Malawi zilipeleka barua ya pamoja kwa jukwaa la marais wa
wastaafu wa nchi za kusini mwa Afrika linaloongozwa Rais Joachim Chissano,
zikiomba zipatanishwe katika mzozo huo baada ya majadiliano ya pande zote mbili
kushindwa kuzaa matunda. Hata hivyo duru za kidiplomasia kutoka Lilongwe
zinasema kuwa, Serikali ya Malawi imejiandaa kuelekea kwenye Mahakama ya Haki
ya Kimataifa(ICJ) iwapo upatanishi huo utashindwa kuzaa matunda.
Gazeti la Daily Times
limewanukuu maofisa wa Serikali wakisema kuwa karata ya mwisho kwa Malawi
itakuwa ni kuelekea kwenye mahakama hiyo ambayo pia imewahi kutoa ufumbuzi kwa
mizozo mbalimbali iliyohusu mipaka.
Mahakama hiyo ya kimataifa
imewahi kushughulikia mzozo wa mpaka uliozihusisha nchi za Cameroon na Nigeria
zilizokuwa zikizozona kuhusiana na eneo lililojulikana Bakassi
Peninsula.Kadhalika imewahi kutatua mzozo wa mpaka baina ya Namibia na Botswana
kuhusiana na kisiwa Kasikil.
 |
Wavuvi wakiwa kazini.. |
 |
Ziwa NYASA hakika ni urithi mzuri.. |
 |
Ziwa NYASA kutoka angani jinsi inavyoonekana... |
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.