Inaarifiwa wafungwa hao walianza kufyatuliana risasi na maafisa wa polisi.
Tukio hilo lilitokea katika mahakama kuu mtaa wa Mthatha katika mkoa wa Eastern Cape.
Mthunzi Mhaga, ambaye ni waziri wa sheria, alisema kuwa mfungwa mmoja alijeruhiwa mguuni wakati wa ufyatulianaji risasi.
''Walijaribu kutoroka walipoingia ndani ya majengo ya mahakama , '' alisema bwana Mhaga.
''Baada ya kuipata bunduki, walianza kufyatuliana risasi na maafisa wa polisi, '' aliongeza kusema bwana Mhaga.
Alisema kuwa polisi waliweza kudhibiti hali.
Kufuatia visa vya hivi karibuni vya ufyatulianaji risasi mahakamani mjini Pretoria na Cape Town, waziri wa sheria alisema kuwa atahakikisha uwepo wa sheria z akudhibiti ulinzi katika majengo ya mahakama.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.