Wataalam wa Marekani,Uingereza na Ufaransa wamewasili nchini Nigeria ili kusaidia kuwatafuta wasichana hao.
Marekani na Uingereza zinasema kuwa zitalipatia kipaumbele ombi la Nigeria la kutuma ndege za upelelezi.
Wakati huohuo Katika tukio ambalo si la kawaida, mke wa rais wa Marekani Michelle Obama anatarajiwa kutoa taarifa ya kila juma ya mumewe itakayoangazia utekaji nyara wa wasichana wa shule nchini Nigeria.
Wake wa marais kwa kawaida hukataa kujihusisha na sera za kigeni ,lakini bi. Obama amekuwa mkosoaji mkubwa wa kundi la wanamagambo wa kiislamu ambao waliwateka nyara wasichana hao.
Awali bi Obama aliweka picha katika mtandao wa tweeter ilio na maneno yanayosema 'Warudisheni wasichana wetu'.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.