Rais wa Nigeria Goodluck Jonathana ameagiza shule
zote na ofisi za serikali katika mji mkuu wa Abuja nchini humo zifungwe
wakati wa siku tatu za Mkutano wa Uchumi wa Dunia World Economic Forum
utakaanza nchini humo jumatano ijayo.
Serikali imesema hatua hiyo ni kuarahisisha
misafara ya magari. Lakini suala la kuimarisha ulinzi huenda ni mambo
yaliyosababisha hatua hiyo Mwandishi wa BBC Will Ross anasema akiwa
Abuja.Ulinzi mkali umehaidiwa kwa wageni wapatao 1000 wakati wa mkutano huo.
Rais Jonathan amesema polisi wapatao 5000 na wanajeshi watafanya doria na kushika hatamu za ulinzi wakati wa mkutano huo utakaoanza wiki ijayo.
"Rais Jonathan amesema polisi wapatao 5000 na wanajeshi watafanya doria na kushika hatamu za ulinzi wakati wa mkutano huo utakaoanza wiki ijayo."
Mji wa Abuja katika siku arobaini zilizopita ulishambuliwa kwa matukio mawili ya mabomu yaliyoua watu wapatao tisini.
Baadhi ya wanawake wakiandama kutaka serikali kuchukua hatua zaidi kuwaokoa wasichana waliotekwa
Kundi hilo hilo pia linatuhumiwa kuwateka nyara wasichana zaidi ya 200 katika shule moja kwenye mji wa Borno uliopo Kaskazini Mashariki mwa Nigeria siku arobaini zilizopita.
Jina la kundi hilo lenye tafsiri ya "Kupiga marufuku elimu ya nchi za Maghiribi" kwa lugha ya Kihausa kimekuwa kikiendesha mashambulizi kadhaa kaskazini mwa Nigeria katika siku za hivi karibuni.
Wanawake walivaa nguo nyekundu kuonyesha kuguswa na wasichana waliotekwa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry ambaye anafanya ziara barani Afrika amesema Marekani itafanya kila liwezekanalo kuisaidia serikali ya Nigeria kuwaokoa na kurudisha nyumbani wasichana mia mbili waliotekwa na kundi la waislamu linalosadikiwa kuwa la Boko Haram siku kumi tisa zilizopita.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.