Amesema kuwa uchaguzi wa Urais uliopangwa kufanywa Mei 25, ni hatua inayofaa.
Siku chache zilizopita Bwana Putin alitaja uwezekano wa kuwa na uchaguzi huo wa Urais kama upuzi mtupu. Lakini katika taarifa ya hivi sasa Bwana Putin amesema uchaguzi huo hautakuwa na maana iwapo raia wote wa Ukraine hawatahusishwa na kuwahakikishia jinsi haki zao zitakavyolindwa baada ya uchaguzi.
Vladmir Putin pia alidai kuwa Urusi imewaondoa wanajeshi wake kwenye mpaka wake na Ukraine.
Hata hivyo mataifa ya Magharibi yanatarajiwa kutoamini hakikisho hili hadi watakaposhuhudia kinachoendelea mpakani.
Mataifa hayo pia yanasubiri kuona iwapo taarifa ya Putin itapunguza uhasama miongoni mwa wananchi wa Ukraine.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.