Wakuu wa makao hayo wanasema kuwa Berlusconi atakuwa tu kama mfanyakazi mwingine yoyote anayefanya kazi katika makao hayo.
Alipowasili, alizomewa na mwanaharakati mmoja akiwamwabia kuwa alipaswa kuwa gerezani.
Hukumu yake mwaka jana ilitokana na kesi ambapo kampuni yake ilinunua haki miliki katika miaka ya tisini.
Lakini aliponea kifungo cha jela kwa sababu mfumo wa sheria nchini Italia unawahurumia sana wazee walio na miaka sabini na zaidi.
Mwandishi wa BBC David Willey anasema kuwa adhabu hiyo itamuwezesha kuendelea kuongoza chama chake Forza Italia, katika uchaguzi wa Ulaya ingawa alilazimika kujiuzulu kutoka katika baraza la Senate.
Berlusconi pia atazuiwa kusafiri katika sehemu nyingi za nchi hiyo baada ya Pasi yake ya usafiri kubanwa.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.