Balozi wa Malawi nchini Tanzania Bi Flossie Gomile
Chidyaonga amefariki dunia mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam
akipelekwa hospitali kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na matatizo ya
maradhi yaliyokuwa yakimkabili.
Taarifa ya wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania
kwa vyombo vya habari imesema "Balozi Chidyaonga aliyekuwa na umri wa
miaka 54 amefariki Ijumaa kutokana na mshipa mkuu wa AORTA kuvimba na
kupasuka kulikosababisha damu kukusanyika kwenye mfuko wa moyo na hivyo
kufanya moyo ushindwe kufanya kazi."
Wizara hiyo imesema, katika kipindi chote
alichokuwa mwakilishi wa Malawi nchini Tanzania, Balozi Chidyaonga
alifanya kazi yake ya kukuza na kuendeleza ushirikiano kati ya nchi
mbili hizo kwa umahiri wa hali ya juu.
Mwili wa marehemu Balozi Chidyaonga unatarajiwa
kusafirishwa Jumanne kwenda Malawi na Jumatano mazishi yamepangwa
kufanyika huko Blantyre.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.