Thursday, July 19, 2012
0

Takriban watu 30 wamefariki dunia baada ya meli iliyokuwa imewabeba abiria zaidi ya mia mbili na hamsini kuzama karibu karibu na kisiwa cha Zanzibar nchini Tanzania .
Kwa mujibu wa taarifa zilizitolewa na kikosi cha wanamaji, watu wengine wengi wanaripotiwa kuokolewa kufuatia meli hiyo kuzama kutokana na dhoruba kali.
Mmoja wa watu waliofika katika eneo kulikotokea ajali hiyo na kushiriki katiia uokoaji ni Mohammed Omar ambaye aliambia BBC kuwa meli hiyo ilikuwa imepinduka na injini zake zikiwa juu: "wengi wa waliookoka ni wale wanaojua kuogoleai na waliokuwa na bahati ya Mwenyezi Mungu."
Mwandishi wetu wa Dar Es Salaam, Hassan Mhelela, ambaye amekuwa akifuatilia ajali hiyo tangu itokee jana amesema shughuli za uokoaji zimeripotiwa kuanza tena.
Alisema zilisimamishwa jana usiku kwa sababu ya hali mbaya ya bahari na giza.
Mwaka mmoja haujakamilika tangu kutokea ajali nyingine kutoka katika njia hiyohiyo ya meli na kusababisha vifo vya mamia ya watu.
Source-bbc..

Mwili ukiopolewa toka majini..

Askari wa Vikosi mbalimbali wakiwa katika kazi ya Uokozi kwa Abiria waliokuwa katika Meli ya Star Gate ambayo ilizama ikiwa imebeba abiria 250 huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar

Waliofariki kutokana na ajali hiyo.....

 
Abiria aliyeokoka katika Meli iliozama ya Star Gate akifarijiwa na Jamaa zake Baada ya kuteremka katika Meli iliyowaokoa hapo Bandarini


Abiria aliyeokoka kutoka katika meli iliyozama...

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, wa pili kulia) akiwa na Viongozi Wakuu wa Serikali alipofika katika Ofisi za Shirika la Bandari.

Watalii na raia wa kigeni pia walikuwemo katika meli iliyozama hawa ni baadhi ya waliosalimika..

Majeruhi wakipatiwa Mablanketi kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kuokolewa...


Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad akiwa katika hali ya huzuni Baada ya kushiriki katika uokoaji

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA