Saturday, June 21, 2014
0
Mwandishi wa habari kijana wa Somalia ameuwawa kwenye mlipuko wa bomu lilotegwa chini ya gari lake mjini Mogadishu.
Yusuf Keynan alikufa wakati bomu hilo lilipolipuka alipowasha gari, akitaka kuelekea kazini.
Mwandishi wa BBC mjini Mogadishu anasema Yusuf Keynan (aliyefanya kazi katika redio Mustaqbal), alikuwa mwandishi wa habari kijana aliyekuwa akipendwa na hodari katika kazi yake.
Huyo ni mwandishi wa habari wa kwanza kuuwawa nchini Somalia mwaka huu, baada ya waandishi habari kadha kuuwawa kwa mfululizo katika miaka miwili iliyopita.
Shirika la Kuwalinda Waandishi wa Habari linasema kuwa Somalia ni moja kati ya nchi hatari kabisa kwa waandishi.
Hata hivyo hakuna aliyedai kuhusika na mauaji ya kijana huyo, hadi hivi sasa..

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA