Thursday, June 12, 2014
0
Uingereza imesisitiza kuwa marufuku iliyowekewa mmea wa Miraa itaanza kutekelezwa tarehe 24 mwezi Juni. Hii inafuatia bunge la nchi hiyo kupitisha uamuzi wa serikali ya Uingereza kuorodhesha miraa katika kundi la dawa za kulevya.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Uingereza imesema kuwa uamuzi huo haulengi Kenya moja kwa moja. Imeongeza kuwa Serikali ya Uingereza imekuwa ikidhamiria kwa muda mrefu kuchunguza kisheria hali ya mmea huo.
Mapema mwezi uliopita wabunge kutoka maeneo ya Meru kunakokuzwa kwa wingi mmea huo walikuwa wametishia kuwasilisha bungeni hoja ya kuwahamisha waingereza wanaomiliki mashamba katika maeneo hayo ikiwa Uingereza itapiga marufuku mmea huo.
Wabunge hao walikuwa wamesema kuwa wakulima wa mmea huo watapata hasara kubwa kwa sababu walikuwa wakiutegemea kukuza uchumi wa eneo hilo.

Na kwa sababu hiyo Uingereza imesema kuwa inatambua matatizo yanayowakumbuka wazalishaji lakini itaendelea kushirikina na serikali ya Kenya kwa kufadhili miradi ya kukuza uchumi.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Uingereza ilichukua uamuzi huo baada ya kushauriana na washiriki wake.
Nchi nyingi zenye uwezo mkubwa wa kiuchumi yaani G8 zikiwemo Canada na Marekani zimeharamisha Miraa iliyotajwa kuwa miongoni mwa dawa za kulevya.
Mswada wa kupiga marufuku mmea huo unaotumia mno Uingereza ulijadiliwa bungeni machi na kuidhinishwa na bunge la chini na lile la juu baadaye hivyo kuwa sheria.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA