Wednesday, June 04, 2014
0
Serikali ya Brazil inapendekeza kuwapa nyongeza ya asilimia 15.8 mishahara polisi wake ili wasigome wakati wa ufunguzi wa michuano ya kombe la dunia wiki ijayo.
Maafisa wakuu wa polisi watapokea nyongeza ya asilimia 12 kuanzia mwezi Julai na nyingine ya asilimia 3.8 mwezi Januari.
Makubaliano hayo yanakuja baada ya mgomo wa polisi mapema mwaka huu ambapo takriban watu 250,000 walishiriki.
Maandalizi ya kombe la dunia ambalo linaanza tarehe 12 Juni, yamekumbwa na maandamano ya kupinga serikali kwa kutumia gharama kubwa kuandaa michuano hiyo.
Polisi ambao hukabiliana na vitendo vya uhalifu na kupambana na ulanguzi wa madawa ya kulevya pamoja na ugaidi, pia watahakikisha usalama mipakani na katika viwanja vya ndege.
'Mgomo wasitishwa'
Chama cha wafanyakazi kinachowawakilisha maafisa hao wa polisi, Fenapef, kimeelezea kufurahishwa na hatua ya serikali kuwaongea mishahara kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia na kabla ya uchaguzi tarehe 5 Oktoba.
Mkuu wa chama hicho alisema kuwa serikali pia imekubali kubuni kikundi cha waakilishi watakaozungumzia swala la kuwapandishwa vyeo polisi waliofika kiwango hicho.
Mwezi jana polisi hao waligoma wakitaka kuongezwa mishahara katika majimbo 14 nchini humo huku walimu na wafanyakazi wa umma pia wakidai mazingira bora ya kazi na nyongeza ya mishahara.
Serikali imeimarisha usalama katika maeneo yote 12 yatakayotumiwa kwa michuano hiyo huku polisi 20,000 wakitarajiwa kudhbiti ulinzi mjini Rio.
Wadadisi wanasema kuwa hatua ya serikali ni kutaka kuhakikisha kuwa maandamano yaliyoshuhudiwa wakati wa kombe la mashirikisho mwaka jana hayatashuhudiwa tena

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA