Tuesday, June 03, 2014
0
Mfalme wa Uhispania Juan Carlos anaachia mamlaka, waziri mkuu Mariano Rajoy ametangaza.
Juan Carlos, mwenye umri wa miaka 76, amekuwa mfalme tangu mwaka 1975 , baada kumrithi aliyekuwa dikteta Francisco Franco.
Mwanawe mfalme, Felipe, 45, ndiye atakayemrithi.
Katika kipindi cha utawala wake, Juan Carlos alionekana kama mfalme mwenye umaarufu sana duniani , lakini hivi karibuni, wananchi wengi wa Uhispania walipoteza imani naye.
Sifa yake imetiwa dosari kufuatia uchunguzi wa muda mrefu wa madai ya ufisadi dhidi ya mtoto wake wa kike na mumewe.
Uungwaji mkono kwa mfalme huyo ulizorota zaidi ilipogundulika kuwa alikuwa katika safari ya kuwinda Ndovu nchini Botswana mwezi Aprili 2012 wakati nchi hiyo ilipokuwa inazongwa na msukosuko wa kifedha.
Mflame Juan amendoka mamlakani kwa sababu zake binafsi.
Hali yake ya kiafya, sio nzuri sana na amefanyiwa upasuaji mara kadhaa katika miaka ya hivi karibuni.
Waziri mkuu hata hivyo alisema kuwa mfalme Juan Carlos amekuwa mtetezi wa haki za watu wa nchi hiyo.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA