Friday, June 06, 2014
0
Bunge la jimbo la jiji la Nairobi nchini Kenya limepiga kura kuwaondoa makahaba katikati mwa mji mkuu.
Waakilishi katika bunge hilo walilazimika kupiga kura mara tatu ili kufikia matokeo hayo. Kwa mara mbili matokeo ya kura yalikuwa sare, lakini baada ya awamu ya tatu kura ya ndio ikashinda.
Hoja hiyo iliwasilishwa na mwakilishi Bi Jane Mwasia, ikitaka wakuu wa jimbo kuwaondoa makahaba mara moja kutoka katikati kwa jiji la Nairobi.
Waakilishi wanaume walipinga hoja hiyo mara tu ilipowasilishwa lakini mjadala ulipotokota, wengi waliamua kupiga kura ya ndio wakati wengine wakijizuia.
Mjadala huo nusura uzue makonde bungeni na kusababisha hisia mseto miongoni mwa waakilishi hao.
Baadhi ya waakilishi hao walipendekeza kuwa sehemu maalum itengewe makahaba hao baada ya wao kundolewa katika barabara zilizo katikati mwa jiji.
"sina tatizo na makahaba kwa sababu wengi wao hawana ajira. Kwa hivyo ni jukumu letu kuwajengea sehemu ambako wataweza kuendeshea shughuli zao,'' alisema mmoja wa waakilishi hao.
Mwakilishi mwingine, Manoah Mboko alisema kuwa suluhu kwa makahaba sio kuwaondoa mjini bali ni kuwaoa kwani sheria ya kuoa zaidi ya mke mmoja ilipitishwa maajuzi. Aliongeza kwamba makahaba wanachangia pakubwa sana katika uchumi wa mji wa Nairobi.
Mwakilishi mwingine alizua kicheko aliposema kuwa dunia nzima ni kama soko na hivyo kila mtu aruhusiwe kuuuza bidhaa zake.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA