Wednesday, October 03, 2012
0
Aliyekuwa bawabu wa Papa Benedict amerejea mahakamani katika kile kinachotarajiwa kuwa siku muhimu kabisa ya kesi yake mjini Vatican kwa mashtaka ya wizi wa....


 nyaraka muhimu za siri kutoka ofisi ya Papa.
Nyaraka hizo zimefichua tuhuma za rushwa na mgogoro wa madaraka katika ngazi ya juu ya Kanisa Katoliki.
Bawabu huyo Paolo Gabriele, anatarajiwa kutoa ushahidi hii leo ikiwa ni siku ya pili ya kesi hiyo.
Makao makuu ya kanisa hilo Vatican wanasema kuwa Gabriele tayari amekiri mashtaka akisema kuwa alitaka tu kuweka hadharani uovu na rushwa ndani ya kanisa hilo.
Bwana Gabriele anakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka minne jela iwapo atapatikana na hatia.
Paolo Gabriele akiwa ameketi mbele, wakati Pope akipungia waumini kutokea ndani ya gari..

Paolo Gabriele, aliyezungushiwa kiduara akimuwekea maji ya kunywa Pope Benedict wa 16, wakati huo akiwa bado kazini.

Paolo Gabriele

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA