Wapiganaji wa kiisilamu wanaodhibiti
sehemu za Kaskazini mwa Mali, wanajipatia pesa kutoka kwa biashara haramu ya
mihadarati na kupitia kwa visa vya utekaji nyara ambapo wanalipwa kikombozi ili
kuwaachilia mateka.
wakati wakitumia sheria ya kiisilamu
katika.......
maeneo wanayodhibiti.
Madai haya ni kwa mujibu wa afisaa
mmoja mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Wapiganaji hao pia wananunua watoto
kuwatumia kama wanajeshi, huku wakilipa familia za watoto hao dola mia sita kwa
kila mtoto. Alisema Ivan Simonovic baada ya kuzuru nchi hiyo.
Wapiganaji hao wenye siasa kali,
walitwaa thuluthi mbili za udhibiti wa Mali, wakati nchi hiyo ilipotumbukia
katika vita baada ya kufanyika mapinduzi ya kijeshi.
Bwana Simonovic alitoa picha ya
kutisha kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanyika katika eneo hilo.
''Haki za wanawake hasa zinakiukwa
pakubwa'' alisema afisaa huyo ambaye ni naibu wa katibu mkuu kuhusu haki za
binadamu katika Umoja wa mataifa ,akielezea kuhusu orodha ya wanawake ambao
hawajaolewa au wale ambao walikuwa wamepata watoto.
Wanawake zaidi wanalazimishwa
kuolewa huku gharama ya kupata mke ikiwa dola elfu moja.
''Visa vya ukiukwaji wa haki za
binadamu hapa ni vya kushtua na vinafanyika sana'' aliambia waandishi wa habari
mjini New York, akiongeza kuwa wapiganaji hao wanatumia sheria kali za
kiisilamu kudhibiti eneo hilo.
Katika ziara ya afisaa huyo ambayo
ilinuia kugundua yanayoendelea nchini Mali, aligundua kuwa wapiganaji hao
wanatumia sheria kali kwa wahalifu.
Hadi kufikia sasa, watu watatu
wamenyongwa hadharani na wengine wanane kukatwa mikono huku wawili wakichapwa
hadharani.
0 comments:
Post a Comment