Thursday, August 21, 2014
0
Utawala wa Saudi Arabia umeagiza kuuawa kwa watu wanne kutoka kwa familia moja kwa kosa la kumiliki dawa za kulevya.
kaka hao waliokuwa katika makundi mawili waliuliwa jumatatu katika mji wa Najran ulio kusini mashariki baada ya kuhukumiwa kwa kupokea kiasi kikubwa cha hashish.
Mahakama ya taifa hilo imetoa adhabu za kifo kwa watu 17 katika wiki mbili zilizopita ikilinganishwa na 17 katika miezi sita ambayo imepita.
Mwaka wa 2013 mamlaka ya Saudi iliadhibu takriban watu 79 watatu wakiwemo chini ya miaka 18 kwa uhalifu huo.

Amnesty International imesema wanaume hao wanne walioadhibiwa wanaojulikana kama Hadi al-Mutlaq, Awad al-Mutlaq, Mufrih al-Yami and Ali al-Yami walikamatawa na kufungiwa na kamati ya jumla ya utafiti ya wizara ya mambo ya ndani mara kadhaa baada ya madai ya uhalifu mwaka wa 2007 .
Wanne hao kama inavyoripotiwa waliteswa kwa kuchapwa, na kunyimwa kulala wakati wa kuhojiwa ili kutoa kukiri makosa yao.
Wizara ya ndani nchini humo ilisema kwamba wanaume hao walipatikana na makosa na mahakama tatu ikiwemo mahakama ya rufaa huku mamlaka ya nchi hiyo ikikanusha kuwa iliwatesa wanaume hao.
Amnesty inasema kuwa huenda wakauawa wakati wowote.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA