Sunday, August 03, 2014
0

Polisi wa Ufaransa wamemkamata afisa mmoja wa kukabiliana na mihadarati kwa kuiba kilo hamsini za Cocaine kutoka makao makuu ya polisi mjini Paris.
Dawa hiyo yenye thamani ya dola millioni 4 ilikuwa imefungiwa katika chumba kimoja baada ya polisi kuipata na genge moja la raia wa Senegal linalofanya oparesheni zake katika mji huo.
Maafisa wanasema kuwa afisa huyo mwenye umri wa miaka 34 alisakwa na kukamatwa katika mji wa kusini wa Perpignan ambapo alikuwa likizo.
katika kesi ambayo imeiletea aibu serikali ya Ufaransa ,polisi walibaini siku ya Alhamisi kwamba dawa hizo zilikuwa zimetoweka katika makao makuu ya polisi.
Taarifa ya polisi inasema kuwa kanda ya video ya CCTV iliomuonyesha mtu mmoja aliyebeba mifuko miwili akiingia katika makao hayo na baadaye akaonekana akitoka na mifuko hiyo.
Afisa huyo mwenye umri wa miaka 34 alipatikana katika mji wa Perpignan ambapo alikuwa akijivinjari.
Waziri wa maswala ya ndani nchini Ufaransa Bernard Cazenueve ambaye amesema kuwa atakabiliana na waliokamatwa bila huruma iwapo itabainika kwamba baadhi ya maafisa walihusika aamesema kuwa afisa huyo tayari amesimamishwa kazi akisubiri uchunguzi.
Mnamo mwezi Aprili maafisa wawili wa polisi walishtakiwa kwa kumbaka mwanamke mmoja raia wa Canada katika jengo hilo.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA