Wednesday, August 13, 2014
0
wezi hao wakiwa kwenye harakati za kupakua pesa.

Wanaume wanane waliokua wamevalia mavazi maalumu meupe na vikaragosi usoni wakiwa na mitutu mkononi walilizuia gari iliyokua ikisafirisha kiasi kikubwa cha pesa mapema wiki hii kikadiriwa kua ni dola milioni kumi za kimarekani sawa na paundi sita nukta mbili za Uingereza. wizi huo umeelezwa kua ni wa kihistoria katika uhai wa taifa la Chile.
Baada ya kulizuia gari hilo, majambazi hao walianza kupakua pesa kutoka katika gari hiyo ambalo ni mali ya jeshi la Marekani na kuziingiza katika gari ya mizigo eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Santiago.
Mashuhuda wanasema kuwa pesa hizo zilikua njiani kupakiwa ndegeni na kupelekwa katika Bank za nchi hiyo na katika machimbo ya madini huko Copiapo,kaskazini mwa Chile.mkanda wa video uliopatikana na polisi dakika mbili baada ya tukio unaonesha genge hilo likiwasili ndani ya mavazi meupe na kujitia ni wamoja kati ya wafanyakazi katika gari hilo ingawa kamera za mahali hapo hazikunasa tukio hilo likitekelezwa.
Waziri wa mambo ya ndani wa Chile Mahmud Aleuy amesema kua polisi katika uwanja huo wa ndege walichanganyikiwa baada ya kuzidiwa maarifa na majambazi hao waliokuwa wamejipanga sawasawa kutekeleza tukio hilo na kusema kua polisi walipaswa kuchukua tahadhari ya hali ya juu wakati fedha hizo zikisafirishwa , na kwamba kazi ya usafirishaji wa vifurushi na mizigo zilikua ni za mamlaka ya anga na sio polisi.
Baada ya kufanikiwa kupora kiasi hicho cha pesa! Majambazi hayo yalijigawa katika makundi mawili tofauti na kuondoka kila moja na njia yake na kusambaza misumari nyuma yake na baadaye gari moja ilitelekezwa na kukutwa tupu jirani na eneo la tukio .
Tukio kama hilo liliwahi kutokea mnamo mwaka 2006,wakati majambazi walipopora dola milioni 1.6 zilizokua zikiingia kusafirishwa katika uwanja huo huo wa ndege, na majambazi wa tukio hilo walikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani ,
Waziri wa ulinzi wa Chile Rodrigo Penailillo ameahidi kua jeshi litaisaidia polisi kuwapata majambazi waliohusika katika tukio hilo.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA