Monday, August 04, 2014
0
Benki ya Taifa ya mbegu za kiume inatarajiwa kuanzishwa nchini Uingereza kuondokana na tatizo la upungufu wa mbegu hizo.
Wapenzi wa jinsia ya kiume na kike , wale wa jinsia moja pia wanawake wasio na wenza watanufaika na huduma hii mpya ambapo kutoka jamii zisizofahamika watakuwa na uwezo wa kuchagua wachangiaji kutoka katika jamii nyingine
Benki hii itakayosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Gamete na Hospitali ya Wanawake ya Birmingham itafunguliwa mwezi Oktoba.

Mradi huu umetengewa paundi 77,000 na Idara ya Afya nchini Uingereza.
Kituo hiki kitakuwa katika hospitali ya wanawake mjini Birmingham ambacho kitakuwa kikihifadhi mbegu hizo.
Hivi sasa kumekuwa na upungufu wa wachangiaji wa mbegu za kiume nchini Uingereza hasa katika hospitali za taifa,huku kukiwa na ongezeko la uhitaji, hospitali hizo zikitibu tatizo hilo linaloelezwa kuwa kubwa nchini humo.
Mfuko huo umesema una matumaini kuwa uwepo wa benki hiyo utapunguza idadi ya wagonjwa wanaojiweka katika hatari kwa kutafuta huduma hii bila kufuata taratibu.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA