Kiongozi wa kanisa katoliki duniani,
Papa Benedict wa kumi na sita amewashukuru waumini kwa maombi yao kwake katika
hotuba yake ya kwanza hadharani tangu....
kutangaza kuwa anajiuzulu
Papa alishangiliwa na maelfu ya watu
alipokuwa anajianda kutoa hotuba yake ya kila wiki mjini Vatican.
Alisema anajiuzulu kwa sababu
anaelewa fika kuhusu hali yake ya kiafya inavyoendelea kudhoofika na
anavyoishiwa na nguvu kutekeleza majiku yake.
Baadaye leo ataongoza misa yake ya
mwisho katika kanisa ya St Peter's Basilica.
Tangazo la kujizulu alilitoa
mwishoni mwa Februari,
Papa mwenye umri wa miaka 85, na
ambaye jina lake kamili ni Kadinali Joseph Ratzinger ataendelea na majuku yake
kama kawaida hadi siku atakapojiuzulu rasmi.
Katika muda wa wiki sita zijazo, Papa mpya anatarajiwa
kuteuliwa.
Akiwa na umri wa miaka 78, kadinali
Joseph Ratzinger, alikuwa mmoja wa Papa wazee zaidi kuwahi kuteuliwa kuongoza
kanisa
Alichukua wadhifa wake wakati ambapo
kanisa lilikuwa linakumbwa na kashfa nyingi ikiwemo visa vya kuwaharibu watoto
vilivyofanywa na makasisi wa kanisa hilo.
|
0 comments:
Post a Comment