Friday, February 08, 2013
0

Askofu aliyedumu kwenye nafasi ya Uaskofu zaidi ya Miongo Mitatu, Askofu Thomas Laizer amefariki jioni ya leo Katika Hospitali ya Rufaa Ya Mkoa wa Arusha. Askofu Thomas Laizer amefikwa na mauti hiyo baada ya kuugua na....


 kukaa Hospitalini hapo zaidi ya mwezi Mmoja.
Askofu Laizer amefariki huku Dayosisi Ya Kaskazini ya Kanisa la KKKT ikiwa inamuhitaji pamoja na busara zake kuweza kutatua mgogoro unaolikabili Kanisa hilo kwa sasa kufuatia deni la mabilioni kadhaa.
Askofu Laizer alianza kuugua mapema mara baada ya mgogoro kuanza kushika hatamu, haijafahamika moja kwa moja kama ugonjwa wa Baba Askofu una uhusiano wa moja kwa moja na mauti iliyomfika.
Baba Askofu Laizer atakumbukwa kwa ujasiri wake  wa kuikosoa Serikali pasipo woga, lakini puia atakumbukwa sana Kipindi cha Babu Wa Loliondo na Kikombe chake Cha Tiba.


STORI HII NI KWA MUJIBU WA S.GOSPEL

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA