Ellinah Wamukoya ameteuliwa kuwa
askofu wa kwanza wa kike wa kanisa la Kianglikana barani Afrika.
Akiongea muda mfupi baada ya kuteuliwa,
Bi. Ellinah Wamukoya amesema uamuzi huo...
heshima kwa kina mama.
Ellinah Wamukoya, 61, sasa atahudumu
kama askofu mpya wa kanisa hilo katika ufakme wa Swaziland, moja wapo ya nchi
zinazokisiwa kufuata siasaa za kihafidina.
Kutawazwa kwake kumejiri huku kanisa
la Kianglikana, likitarajiwa kujadili ikiwa kina mama wataruhusiwa kuapishwa
kuwa maaskofu wa kanisa hilo.
Askofu wa jimbo la Capte Town,
nchini Afrika Kusini, amesema kuwa wamechukua uamuzi huo ili wawe mfano kwa
wengine na pia kuwatakia, viongozi wa kanisa hilo, faraja na hekima ili
kujadilia sauala hilo kwa haraka.
Kwa mujibu wa ripoti aliyotuma kwa
vyo,bo vya habari, askofu huyo wa jimbo la Cape Town, Revd. Thabo Makgoba,
amesema wimbi kwa sasa linavuma na kuwa wameshuhudia tukio la kihistoria ambao
ni sawa na bingu kufunguka.
David Dinkebogile aliongoza sherehe
hizo na kukariri kuwa nia yao kuwa ilikuwa kumuapisha askofu na wale sio mtu
mweusi, muafrika na raia wa Swaziland.
Askofu Wamukoya ni meya wa zamani wa
mji mkuu wa Swaziland Manzini.
|
0 comments:
Post a Comment