Monday, November 19, 2012
0


"Iron Dome" ni mmojawapo ya kinga nyingi inayomilikiwa na Israel, na inayotumika dhidi ya makombora.
Mfumo huo unatumia rada ili kufuata makombora yanayorushiwa Israel, halafu...
 
 hufyatua makombora yake ili kuangamiza hayo yanaoyojaribu kupenya.
Mfumo huu ulichukua miaka mingi kujenga na ulianza kutumika mapema 2011.
"Iron Dome" imesifiwa sana na jeshi la Israel katika mashambulizi yanayoendelea huko Gaza.
Ilipofika Jumamosi iliyopita jioni, kinga hiyo ilikuwa imeshazuia makombora 245 toka Gaza katika muda wa siku tatu, kulingana na habari za kijeshi.
Hata hivyo inaonekana kwamba wapinzani wa Gaza wanazidi kuboresha silaha zao.



0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA