Askofu wa Durham, Justin Welby,
ambaye pia ni mfanyakazi wa zamani katika sekta ya mafuta, anatarajiwa kutajwa
kama askofu mpya wa...........
Canterbury.
Inaaminiwa kuwa askofu huyo, mwenye
umri wa miaka 56, atateuiliwa kuchukua nafasi ya askofu Rowan Williams,
atakayeachia ngazi mwezi Disemba baada ya miaka kumi uongozini.
Askofu Welby, aliteuliwa kama askofu
mwaka mmoja uliopita alipochukua wadhifa wa nne kwa ukubwa katika kanisa la
kianglikana nchini Uingereza.
Duru kutoka makao makuu ya waziri
mkuu nchini humo, zinasema kuwa askofu huyo atatangazwa rasmi siku ya Ijumaa.
Mnamo Jumanne, wadadisi waliwacha
kubahatisha kuhusu nani atachukua wadhifa huo baada ya watu wengi kutabiri kuwa
yeye ndiye atachukua nafasi ya Rowan Williams
Jarida la Daily Telegraph, lilinukuu
kuwa Askofu Welby amekubali kuchukua wadhifa huo ingawa kwa sasa hangeweza
kutoa tamko lolote kuhusu udadisi juu yake.
Askofu Welby alisomea chuo kikuu cha
Cambridge na kisha kufanya kazi katika sekta ya mafuta kwa miaka kumi na moja
kabla ya kusomea dini ambapo baadaye alitawazwa mwaka 1992.
Askofu Justin Welby |
Akiwa pamoja na Malkia Elizabeth wa UK.. |
0 comments:
Post a Comment