Tuesday, August 14, 2012
0
Wanamuziki nguli katika kazi ya MUNGU, Kirk Franklin, Marvin Sapp, Donnie McClurkin na Israel Houghton kwa pamoja wamewaomba mashabiki wote wa muziki wa “gospel” kuonesha mapenzi makubwa kwa muziki huo na kwa waimbaji ili kuzidi kuwatia moyo katika kazi hiyo.
Kwa pamoja “manguli” hao wameamua kufanya ziara kubwa ya miji zaidi ya kumi na sita huko Marekani, ambayo itaanza Septemba 16, katika Jimbo la Phoenix. Tuna matumaini makubwa pia ya kuwashirikisha waimbaji wa “mama” kama vile MARY MARY na YOLANDA ADAMS, aliongeza Kirk Franklin.
“Ziara hii itafungua milango na kuhamasisha vipaji vingine huko vilipo, najua haitokuwa rahisi, lakini tupo tayari na tumejitoa kwa hilo kwa asilimia 100” alimalizia kusema Kirk Franklin.
Changamoto kubwa pia kwa waimbaji wa “gospel” Tanzania, je tuna upendo kati yetu, je tunafikiria kuinua vipaji vipya?  TAFAKARI na BARIKIWA.


Kutoka kushoto ni Donnie McClurkin, Israel Houghton, Marvin Sapp na Kirk Franklin..


Kutoka kushoto ni Israel Houghton, Donnie McClurkin, Kirk Franklin na Marvin Sapp..  



Hawa ndio Mary Mary, ambao nao wataambatana na kina Franklin kwenye tamasha la zaidi ya miji 16.. kuanzia Septemba 16 baadae mwaka huu!



Yolanda Adams, naye pia ataongozana na Mary Mary pamoja na kina Franklin, katika ile zira ndeeefu! Natamani hata hapa kwetu pia ifanyike jamanii! Lets do this.. Stara Thomas, Shusho, John Lissu "mnyampaha", Frola Mbasha, Jordan River, The Voice na wengine!


 


Yolanda Adams akiwa na tuzo yake, kutoka BET ambayo ametunukiwa mwaka huu..

Hawa ni Mary Mary.. Wamependeza? na wewe unataka kupendeza? Njoo kwa YESU! Utapendeza milelee..


Mary Mary, sifa na utukufu kwa Bwana!

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA