Kwenye mkutano na wandishi habari rais Al-sisi alisema kuwa kuhukumiwa kwa waandishi hao kumeonyesha picha mbaya kuhusu Misri.
Waandishi hao walihukumiwa kifungo cha kati ya miaka 7- 10 gerezani kwa kueneza habari za uongo na kulisaidia kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood.
Muda mfupi baada ya hukumu hiyo rais Al sisi alisema kuwa hawezi kuingilia shughuli za mahakama
Nduguye Peter Greste Andrew amesema kuwa matamshi hayo yamempa matumaini.
Naye nduguye Mohammed Fahmt amesema kuwa hii ni ishara kwamba jambo fulani ni lazima lifanywe.
Lakini familia ya mwandishi mwingine wa tatu aliye kizuizini Baher Mohammed ilipuunza matamshi hayo na kuyataja kuwa ya kuchekesha.
Waandishi hao wote watatu wanajipanga kukata rufaa
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.