Neymar aligongwa upande wake wa nyuma dakika tano tu kabla ya mchuano huo wa robo fainali kukamilika.
Alibebwa na kutolewa nje akiwa katika machela lakini ametolewa hospitalini baada ya kufanyiwa matibabu.
Brazil pia itaendelea kushiriki katika mashindano hayo bila nahodha wake Thiago Silva katika mchuano wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo kupewa kadi ya pili ya Njano.
Kabla ya habari hizo za Neymar kutolewa raia wa Brazil walifurika katika barabara za taifa hilo kusherehekea ushindi wa timu yao.
Katika robo fainali ya kwanza Ujerumani iliishinda ufaransa kwa bao moja kwa bila
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.