Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis
amesema kuwa anaamini sheria inayowazuia makasisi katika kanisa hilo
kuoa huenda ikaondolewa kulingana na wakati.
Papa Francis amesema kuwa sababu za kuiondoa sheria hiyo ya miaka elfu moja na mia moja ipo na kwamba atazitafuta.
Katika mahojiano na gazeti la kitaliano ,la Republica ,papa Francis pia ameifananisha na ugonjwa wa ukoma hatua ya makasisi kuwanyanyasa kimapenzi watoto wadogo.
Amesema kuwa takriban asilimia mbili ya viongozi hao wa dini ikiwemo maaskofu pamoja na makadinali huwanyanyasa watoto kimapenzi,na kwamba yuko tayari kukabiliana na tatizo hilo kwa hali na mali.

0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.