Wanasayansi hao waligundua hili kwa kuwafuatilia na kuwanasa kwa video Sokwe nchini Uganda na kutathmini zaidi ya visa 5000 vya umuhimu wa mawasiliano hayo.
Matokeo ya utafiti huu yamechapishwa katika jarida la Bayolojia ya kisasa.
Daktari, Catherine Hobaiter, aliyeongoza utafiti huo, alisema kuwa huu ndio mfumo pekee wa kimataifa wa mawasiliano kuhusu wanyama kuwahi kurekodiwa.
Ni binadamu pekee na Sokwe ambao wana mfumo wa mawasiliano ambapo walitumiana ujumbe kwa lengo fulani
''Hicho ndicho kitu kimetushangaza sana kuhusu ishara zinazotumiwa na Sokwe katika mawasiliano yao,'' alisema mtaalamu huyo.
Hawa ndio wanyama pekee wanaosalia kuwa na mfumo sawa wa mawasiliano na binadamu. '' aliongeza daktari huyo.
'Mayowe au ishara?'
Mwanzo Sokwe watahakikisha kuwa ujumbe umeweza kumfikia mnyama anayetakikana.
Hii ilikuwa tofauti kubwa kati ya kupiga mayowe na kutoa ishara kwa mnyama fulani, kulingana na daktari Hobaiter.
Hata hivyo, watafiti wanasema kuwa inshara zinazotolewa na Sokwe, hazieleweki vyema , ingawa hizo ndizo hutumika zaidi kwa mawasiliano yao.
Mfano kula majani kwa wanyama hawa huwa ni ishara ya kutaka kujamiiana,
Katika moja ya kanda ya video, Sokwe mama anamnyonyea mguu mtoto, ishara ya kumtaka kupanda katika mgongo wake ili watembee pamoja.
Sokwe ni wanyama wanaoonekana kuwa na ukaribu mkubwa na binadamu hasa kwa wanavyowasiliana.
Mmoja wa watafiti wa utafiti huo alisema kuwa utafiti wenyewe ulikuwa muhimu sana katika kutaka kuelewa mchipuko wa mawasiliano miongoni mwa binadamu.
Lakini alisisitiza kuwa matokeo hayakufichua mengi waliyoyataka.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.