
Mashabiki wawili wauawa Kenya kufuatia ushindi wa Brazil dhidi ya Colombia
Furaha ya mashabiki wawili wa
kombe la dunia iligeuka na kuwa matanga jumamosi usiku baada ya watu
wawili kupoteza maisha kufuatia ubishi kuhusiana na matokeo ya kombe la
dunia linaloendelea huko Brazil.
Shabiki wa kwanza aliuawa baada ya utani wa
shabiki ilizusha ubishiuliyosababishwa akadungwa kisu tumboni nje ya
baa moja katika mtaa wa Awendo iliyoko katika jimbo la Migori magharibi
mwa Kenya.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo
hilo,Kipsang Chengach alisema kuwa wawili hao walikuwa washabikia timu
hasimu katika mechi hiyo ya robo fainali kati ya Brazil na Colombia na
baada ya Brazil kushinda mmoja akamdunga mwenzake kisu na kisa
akatoroka.
Zaidi ya Saa nane baadaye yule aliyetoroka eneo
la tukio naye alisakwa na umati wa watu waliokuwa wamejawa na hamaki na
wakampiga hadi kufa kabla ya polisi kufika huko alikokuwa ametorokea.
Mashabiki wawili wauawa Kenya kufuatia ushindi wa Brazil dhidi ya Colombia
Shabiki mmoja aliyeshuhudia matukio hayo
aliwaambia polisi kuwa alishuku alikuwa ameweka dau na akashindwa kulipa
baada ya mechi hiyo ambayo Brazil iliibuka washindi mabao 2-1.
Miili yote miwli imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.