Mwanamume mmoja nchini Marekani
alimuokoa dereva wa gari ,lililokuwa linateketea kwa kuukunja mlango wa
gari hilo kwa mikono yake.
Polisi wamemtaja Bob Renning, mwenye umri wa miaka 52,kama mtu mwenye nguvu za ajabu.Alianza kwa kuegesha gari lake kando ya barabara kuu mjini Minnesotaili kumsaidia dereva huyo ambaye alikuwa ndani ya gari lililokuwa linateketea.
Bwana Rob aliwaambioa wandishi kuwa haelewi alivyoukunja mlango wa gari hilo kiasi cha kuvunja dirisha la gari.
"alifanya kitendo cha ajabu , kuukunja mlango wa gari hilo lililokuwa linateketea ili kumuokoa dereva, '' alisema polisi.
Dereva wa gari hilo alisema hakuwa na habari ikiwa kuna mtu alikuwa anamuokoa.
Alipatwa na tatizo la kupumua kutokana na moshi mkubwa uliokuwa unafuka ndani ya gari lake , ingawa aliokolewa kupitia kwa dirisha la mlango huo uliokuwa umevunjwa.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.