Monday, September 08, 2014
0


Maafisa wa utawala nchini Misri, wamewakamata wanaume saba baada ya kuonekana kwenye kanda ya video ya harusi ya wapenzi wa jinsia moja.
Kanda hiyo iliyokuwa inaonyesha kikundi cha wanaume wakisherehekea juu ya boti katika mto wa Nile, ilisambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Wanaume hao wanakabiliwa na mashitaka ya kuchochea tabia mbaya na kusambaza picha ambazo zinakwenda kinyume na maadili ya umma.
Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na sheria nchini Misri, lakini wanaume wanaopatikana na hatia hushitakiwa kwa kosa la kudharau dini na kuvunjia jamii heshima.
Mnamo mwezi Aprili wanaume wanne walikamatwa na kufungwa jela kwa kuvunja sheria za kusisitiza maadili mema katika jamii.
Idadi kubwa ya wanaume walikamatwa mwaka 2001, na kushitakiwa kwa makosa sawa na hayo.
Viongozi wa mashitaka waliamuru uchunguzi wa kimatibabu kwa wanaume hao saba ili kuweza kubani msimamo wao wa kimapenzi.
Uchunguzi kama huo hufanywa mara kwa mara nchini Misri, lakini mashirika ya kutetea haki za binadamu huyapinga na kusema yanakwenda kinyume na haki za binadamu.

0 comments:

Post a Comment

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA