Mahakama ya kikatiba nchini
Uganda imefutilia mbali sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ambayo
ilisababisha mataifa ya magharibi kuinyima msaada.
Kadhalika sheria hiyo ilizua gumzo sana sio tu
Uganda bali kote duniani ambapo mataifa ya Magharibi yalilazimika
kuingilia kati.
Mahakama ilisema kuwa mswada huo kabla ya
kuidhinishwa kuwa sheria ulipitishwa na wabunge ambao idadi yao
haikutosha kupitisha mswada na kwa hivyo ni kinyume na sheria.

Baadhi ya waandamanaji waliounga mkono serikali kwa kuharamisha mapenzi ya jinsia moja
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja, tayari
vilikuwa vimeharamishwa Uganda , lakini sheria hiyo mpya pia
iliharamisha hatua zozote za kueneza mapenzi ya jinsia moja na wakati
huu hata kuwajumuisha wanawake wasagaji kama sehemu ya wapenzi wa jinsia
moja.
Mataifa kadhaa ya Magharibi yamesitisha msaada kwa Uganda hasa baada ya sheria hiyo mpya kupitishwa.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.