Sunday, August 24, 2014
0
Mchezaji mpira kutoka Cameroon amefariki baada ya kupigwa kichwani wakati mashabiki wakorofi waliporusha mawe mwishoni mwa mechi ya ligi ya Algeria.
Albert Ebosse, aliyekuwa na umri wa miaka 24, ndiye aliyefunga magoli mengi  katika ligi ya Algeria msimu uliopita.
Alirushiwa kitu wakati mashabiki walipokerwa kwa timu yake, JS Kabylie, ilipofungwa kwa magoli mawili kwa moja katika mechi iliyochezwa nyumbani, Tizi Ouzou yeye ndiye aliyefunga hilo goli moja kwa timu yake.
Wizara ya mambo ya ndani ya nchi ya Algeria imeamrisha uchunguzi ufanywe.
Ligi ya Algeria imefunga uwanja wa mpira wa timu ya JS Kabylie na imeitisha mkutano wa dharura Jumatatu.

0 comments:

Post a Comment

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

MAONI YAKO HAPA

Name

Email *

Message *

MARAFIKI

WANAO NITEMBELEA

66198