Raia wawili wa Misri wameuawa na
wengine wawili kujeruhiwa, kwenye shambulio liliotekelezwa dhidi ya kanisa moja
la Coptic mjini Misrata.
Afisa mmoja wa baraza la mji huo
ameiambia......
BBC kuwa kumetokea mlipuko ndani ya jengo la kanisa hilo wakati wanne
hao walipokuwa wakila chakula chao cha mchana.
Haijulikani ni nani aliyefanya
shambulio hilo mjin Dafiniyah, viungani wa Misrata.Hata hivyo kuna habari za
kutatanisha kuhusu ni lini shambulio hilo lilitokea.
Afisa huyo asema kanisa hilo
lilishambuliwa kwa bomu la kujitengenezea, kwa kuwa baruti zinazotumika kwa
uvuvi zilipatikana katika eneo hilo
Shirika la habari la serikali
limesema kuwa, serikali ya nchi hiyo imeagiza maafisa zaidi wa polisi kutumwa
katika kanisa hilo.
Waziri wa mambo ya nje wa Misri,
Mohammed Kamel Amr, amesema, serikali imeagiza uchunguzi kufuatia tukio hilo na
kusema waliohusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Kanisa hilo lililoka katika eneo la Dafiniyah,
nje kidogo ya mji wa Misrata, hutumiwa na raia wengi wa Misri.
Kuna idadi ndogo sana ya wakristu
nchini Libya, wengi wao wakiwa raia wa kigeni.Baadhi yao wahamiaji kutoka Misri
ambako waumini wa kanisa la Coptic ndilo dhehebu kubwa zaidi la Kikristo.
Serikali ya Libya imekuwa
ikikabiliana na matatizo wa kuhakikisha usalama tangu kuondolewa madarakani wa
kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mwaka uliopita.
Katika siku za hivi karibuni
kumekuwa na mashambulio ya kigaidi dhidi ya majengo ya kibalozi na yale ya
mashirika ya kutoa misaada na mwezi Septemba mwaka huu, Ubalozi wa Marekani,
mjini Benghazi ulishambuliwa na balozi wa Marekani na maafisa wengine waliuawa.
0 comments:
Post a Comment